Alhamisi, 10 Julai 2014

JOINING INSTRUCTION SHULE YA SEKONDARI MWENGE - SINGIDA

                                        JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                                     WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
                                         HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA
                                                  SHULE YA SEKONDARI MWENGE
                                                                     S. L. P. 195
                                                                       SINGIDA
                                                               SIMU 026 250 2093

KUMB. NA. MSS/ C / FV/SL Tarehe: 01/07/2014.

MZAZI/MLEZI WA _____________________________
S.L.P.______________________________
___________________________________
YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA ____________________
Ninayo furaha kukuarifu kuwa mwanao___________________________________________ amechaguliwa kujiunga Kidato cha Tano hapa Mwenge Sekondari kwa masomo ya tahsusi ya ____________________________
Ni matumaini yetu kuwa wewe Mzazi / Mlezi utashirikiana na Uongozi wa Shule katika malezi ili Mwanao aweze kuitumia nafasi hii ya Elimu ya juu ya ngazi ya Sekondari kwa manufaa yake na Taifa kwa ujumla.
Shule yetu itaanza/itafunguliwa kwa masomo tarehe 14/07/2014 Ili kuwezesha usajili kufanyika kwa ukamilifu, mwanao anashauriwa kufika shuleni siku mbili kabla ya siku hiyo.
Mzazi / Mlezi ni wajibu wako kulipa karo ya Shule na michango iliyokubalika na Bodi ya Shule. Ieleweke kuwa siyo jukumu la Mkuu wa Shule kusamehe kulipa karo bali wewe Mzazi / Mlezi ufanye mipango ya kupata mlipa karo (Mfadhili) mapema vinginevyo mwanao atapata usumbufu wa kurudishwa nyumbani kufuata karo ya Shule. hapa chini.
1. MCHANGO WA ADA TSHS. 70,000/= kwa mwaka, au Tshs. 35,000/= kwa muhula. UTALIPA KWENYE A/C No. 5081100022 Jina la akaunti ni MWENGE SECONDARY SCHOOL EDUCATION DEVELOPMENT A/C.
MICHANGO MINGINE YOTE TSHS.179000/= UTALIPA KWENYE AKAUNTI 5081100036 Jina la akaunti ni SCHOOL SELF Mara baada ya Mwanafunzi kufika Shuleni, anatakiwa kuripoti kwa msajili kabla ya saa 11:30 jioni. &nbsp ; &nbsp ; MWANAO HATAANDIKISHWA SHULE BILA KUKABIDHI OFISINI FOMU ZOTE ZA USAJILI ZILIZOJAZWA KIKAMILIFU, ZILIZOAMBATANISHWA KATIKA BARUA HII YA KUJIUNGA. (Uk. 7, 8, 9 na 10). Hairuhusiwi kuwepo Shuleni bila kusajili.
(A) MAHALI SHULE ILIPO
Shule ya Sekondari Mwenge ipo katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida mjini. Usafiri wa kufika Singida ni kwa usafiri wa basi.
(B) ADA NA MICHANGO
Fedha zote zilipwe kwenye Benki kwa maelezo ya namna ya kulipa yaliyotolewa hapo chini. Hati ya malipo (BPS) iandikwe jina na kidato (Mfano: Juma James F.5 HGL) nyuma ya BPS hiyo. Mwanafunzi alete Shuleni
“Original Bank Pay – in Slips” (BPS) mbili siyo photocopy. BPS hizo amkabidhi MHASIBU WA SHULE wala siyo Mwanafunzi yoyote. Mchanganuo wa malipo ni kama ifuatavyo:-
(i) Kukodi godoro la shule Tshs. 5,000/= kwa muhula.
NB: Mwanafunzi haruhusiwi kuja Shuleni na godoro lake binafsi.
(ii) SARE ZA SHULE (Suruali mbili za rangi ya jungle green, mashati 2 ya mikono mirefu; Tshirt (1), Tai (1) na sweta rangi ya jungle green 1).

Utazipata Shuleni kwa kulipia jumla ya Tshs. 80,000/=
(iii) Ada kwa mwaka ------------------------------ Tshs. 70,000/=
(iv) Fedha za tahadhari -------------------------- Tshs 10,000/= (kwa miaka miwili)
(v) Kitambulisho --------------------------- Tshs. 5,000/= (Ni pamoja na picha 4)
(vi) Nembo ya shule ---------------- Tshs.4,000/=
(vii) Matibabu -------- Tshs. 10,000/=
(viii) Kuimarisha taaluma ---------------Tshs. 15,000/=
(ix) Ulinzi --------------------------Tshs. 15,000/= kwa mwaka
(x) Mchango wa madawati----------------------------------Tshs. 25,000/=
(xi) Ukarabati mdogomdogo ------------------------Tshs. 10,000/=kwa mwaka
JUMLA Tshs. 249,000/=
(C)SARE NYINGINE
(i) Viatu vyeusi vya ngozi vyenye kamba na vyenye visigino vifupi. Dawa ya viatu nyeusi na brashi.
(ii) Soksi nyeusi jozi mbili.
(iii) Sare za kazi na michezo: bukta ya bluu, suruali mbili za kitambaa cha khaki zisizobana na sio za mtindo wa ” Jeans”.
(iv) Shuka “light blue” jozi moja
(v) Blanketi moja
(vi) Chandarua ya ukubwa wa futi 3
NB: HAKIKISHA KUWA MWANAO ANALIPA TSHS. 214,000/= KATI YA JUMLA YA TSHS 249,000/= MARA ANAPOKUJA SHULENI KWA MARA YA KWANZA KWA AJILI YA KUANDIKISHWA SHULE.
NAMNA YA KULIPA MICHANGO MBALIMBALI YA SHULE – 2013 KUPITIA BENKI (NMB)
2. Michango ya Shule italipwa kama ifuatavyo REALIANCE A/C.
Tafadhali zingatia utaratibu huu bila kukosea na Bank Pay – in Slips mbili za akaunti hizo uje nazo Shuleni.
(D) VIFAA VYA SHULE
(i) Ream 1 ya karatasi za photocopy A4 kuletwa Shuleni kila mwanzo wa mwaka wa taaluma.
(ii) Vifaa viwili vya usafi ni:-
1) CBG + EGM - Rubber Squeezer na Slasher
2) HGE - Rake na Hard Broom
3) HGK + HGL - Soft broom + Ndoo lita 10
4) HKL - Panga na Ndoo lita 10
5) PCB + PCM - Jembe na Ufagio wa Chelewa
(iii) MAHITAJI YAKE BINAFSI
(i) Fedha za matumizi pamoja na dharura kwa matibabu. Ni vizuri akifungua Akaunti.
(ii) Taulo, ndala, mswaki, dawa ya mswaki, sabuni za kufulia na kuogea, ndoo ya lita 10 na chombo cha kutunzia maji ya kunywa. (Galoni lita tano)
(iii) Sahani, bakuli, kijiko.
(iv) Madaftari makubwa (counter books) 8 (Quire No. 3) za kutosha, kalamu na pencils.
(v) Scientific calculator kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi Hisabati na Jiografia.
(vi) Faili moja kwa kila somo kwa ajili ya kutunzia vitini (Handouts) mbalimbali na karatasi zake za majaribio na mitihani ya muhula. Yatakuwa yakikaguliwa.
(vii) Uingiapo Kidato cha Sita mwanafunzi atalazimika kutoa mchango wa Mtihani wa Mock. Atajulishwa gharama.



(E) MATIBABU
Matibabu yanafanywa kwenye kituo cha afya hapa mjini kwa kutumia mpango wa tiba kwa kadi (TIKA). Kwa magonjwa yanayohitaji fedha nyingi hakikisha unazo fedha nyingi za kugharamia matibabu.

(F) Wanafunzi wa machaguo (Combinations) ya sayansi na ya uchumi kutoa wa PCM na EGM wote wanalazimika kusoma somo la Hisabati la BAM (Basic Applied Mathematics).Hao ni pamoja na wa HGE.

(G) KUBADILISHA COMBINATION:
Shule hii ina combinations zifuatazo: PCM, PCB, CBG, EGM, HGE, HGL, HGK na HKL.
Kubadilisha combination kutaruhusiwa ndani ya siku 30 tu tangu siku ya kufungua Shule.
NB: LAZIMA UJE NA BARUA YA MZAZI / MLEZI WAKO YA KUKURUHUSU
KUBADILI “TAHSUSI” COMBINATION.
(H) MIPAKA YA SHULE

1. (i) Mipaka ya Shule iko wazi na utakapofika hapa utaiona / utaonyeshwa.
(ii)Hairuhusiwi kutoka nje ya mipaka hiyo bila kibali na lazima Mwanafunzi avae sare za Shule akitoka nje.
(iii)Saa za kutoka nje ya mipaka hiyo zimeonyeshwa kwenye ratiba ya siku.

2. Wanafunzi hawaruhusiwi kutembelea sehemu zifuatazo isipokuwa kwa kibali maalumu:-
(a) Chumba maalumu cha waalimu (Staff room).
(b) Ofisi za Shule (School Office).
(c) Maabara na karakana
(d) Jikoni
(e) Nyumba za Walimu na Wafanyakazi wasio Waalimu.
3. Hairuhusiwi kuhama bweni ulilopangiwa bila ruhusa.

(I) SEHEMU AMBAZO MWANAFUNZI HARUHUSIWI KUONEKANA
Ni marufuku kuonekana sehemu zifuatazo
(a) Vilabu vya pombe (Bar na night clubs).
(b) Majumba ya starehe (Cinema halls, Disco halls n.k.)
(J) Masomo yote isipokuwa somo la Kiswahili yanafundishwa kwa lugha ya kiingereza. Anashauriwa kufanya juhudi za makusudi kujifunza lugha hiyo ya mawasiano.

(K) Ni lazima kila Mwanafunzi kushiriki katika mchezo mmojawapo kati ya michezo iliyopo Shuleni.


(L) Kama utasomeshwa na Halmashauri ya Wilaya / Manispaa yoyote Tanzania au na mfadhili yoyote yule uje Shuleni na barua ya mfadhili huyo ya kukubali kukusomesha.

(M) LIKIZO
Mwanafunzi haruhusiwi kubaki Shuleni wakati wa likizo. Hivyo mzazi hakikisha kuwa unamtumia mwanao fedha za kutosha kwa ajili ya nauli wakati Shule inapokaribia kufungwa.

(N) SHERIA NA KANUNI MUHIMU ZA SHULE
Shule inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya elimu Na. 25 ya mwaka 1978. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na Wizara mbili (TAMISEMI na MOEVT) zenye dhamana ya Elimu nchini. Unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo:-
(a) Heshima kwa Viongozi. Wazazi, wafanyakazi wote, wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla ni jambo la lazima.
(b) Mahudhurio mazuri katika kila shughuli ndani na nje ya shule ni muhimu.
(c) Kutimiza kwa makini maandalio ya jioni. (Preparation).
(d) Kuwahi katika kila shughuli za shule na nyingine utakazopewa.
(e) Kufahamu mipaka ya shule na kuzingatia kikamilifu maelekezo juu ya kuwepo ndani ya mipaka hiyo wote awepo shuleni.
(f) Kutunza usafi wa mwili na mazingira ya shule.
(g) Kuvaa sare za shule wakati wote na kwa mujibu wa taratibu na maelekezo.
(h) Kuzingatia ratiba ya shule wakati wote.

(O) MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULENI
1. Wizi
2. Uasherati, ubakaji na ushoga
3. Uvutaji bangi
4. Matumizi ya pombe au madawa ya kulevya kama vile bangi, cocaine, mirungi, kuberi n.k.
5. Kupigana au kupiga.
6. Kuharibu kwa makusudi mali ya Umma.
7. Kudharau bendera ya Taifa.
8. Kuoa / Kuolewa
9. Kusababisha mimba ndani na nje ya shule.
10. Kupatikana na simu ya mkononi shuleni.
11. Kugoma, kuchochea na kuongoza au kuvuruga amani na usalama wa shule na watu kwa ujumla.
12. Kukataa adhabu kwa makusudi.


MAMBO MENGINE MUHIMU YA KUJA NAYO
(a) Medical Examination form ambayo itajazwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Serikali. Fomu hii itakabidhiwa kwa Mkuu wa Shule mara utakaporipoti Shuleni.
(b) Fomu ya maelezo binafsi kuhusu historia ya Mwanafunzi / mkataba wa kutoshiriki katika migomo, fujo na makosa ya jinai.
(c) Fomu ya Mzazi / Mlezi kukiri kukubaliana na sheria na kanuni za Shule, kulipa ada na michango mingine, pamoja na maelekezo mengine yatakayotolewa na Shule.
(d) Nakala na cheti cha kuzaliwa (Birth certificate) nakala halisi ya matokeo yake.
(e) Mwanafunzi lazima aje na RESULTS SLIP original pamoja na nakala kivuli moja. Aidha mwanafunzi haruhusiwi kubadilisha jina lake mahali popote na wakati wowote awapo Shuleni.

KARIBU SANA MWENGE SEKONDARI


_______________________
BONUS P. NDIMBO
MKUU WA SHULE.













Jumatano, 5 Februari 2014

KAMA WEWE NI REGIONAL TRAINER, AU NATIONAL FACILITATOR NA UNA PICHA AU TAARIFA  AU MAONI, TUWASILIANE KWA godfreyp36@gmail.com


Tuwajibike, Tujitume kwa Maendeleo ya Elimu Tanzania


MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA SASA


TANGA KUNANI PALE


PARTICIPANTS  AT USAGARA SECONDARY SCHOOL, TANGA 

Usagara Secondari, Tanga


From left, Dr Tilya President SMASE Tanzania, third from left Coordinator from Ministry of Education Doroth M and National Facilitors.